Barua pepe: kikosimaalum64@kmkmzanzibar.go.tz  |  S.L.P: 565

Logo
Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar
Logo

Mnamo Tarehe 20 Agosti, 2013 Mhe. Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein alifanya mabadiliko ya baadhi ya Wizara ambayo yamepelekea kubadilika kwa miundo ya baadhi ya wizara hizo pamoja na watendaji wakuu.
Katika mabadiliko hayo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maaluum SMZ imeundwa rasmi. Maeneo makuu ya wizara hii ni:

  1. Mamlaka ya serikali za Mikoa na Mitaa
  2. Vitambulisho vya ukaazi (Sasa inajulikana kama Ofisi ya Usajili wa Matukio ya kijamii)
  3. Idara Maalum za SMZ

Pia Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ibara ya 121 imetoa mamlaka kwa muheshimiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuunda Idara Maaluum ikiwemo Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) Zanzibar.

Aidha kwa mujibu wa ibara ya 123(1) Kamanda Mkuu wa Idara Maalum za SMZ ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Na Waziri wa nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum SMZ ndie Msimamizi wa wizara inayosimamia idara maalum za SMZ.


Kikosi cha Wanamaji Zanzibar (Zanzibar Navy) ambacho asili yake ni Idara ya Usalama Zanzibar kilikuwa na madhumuni ambayo ni kulinda uhuru wa Zanzibar (ambao ulipatikana kwa mapinduzi ya 1964) pamoja na mipaka ya baharini ya Zanzibar na watu wake. Mnamo tarehe 01/07/1973 Kikosi cha Wanamaji Zanzibar kilibadilishwa jina na kuitwa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), mbali ya kubadilishwa jina lakini malengo na madhumuni yake yalibaki kuwa yale yale.

Ni kuwa na Kikosi bora na cha kisasa chenye uwezo wa kulinda mipaka ya bahari ya Zanzibar.
Malengo haya yanathibitishwa na kauli ya aliye kuwa Raisi wa kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee. ABEID AMANI KARUME pale alipokuwa akiwaaga vijana wa kundi la kwanza kwa safari ya kwenda mafunzoni nchini Ujerumani Mashariki aliposema
".....Vijana mkasome usiku na mchana maana nchi haina ulinzi wa kutosha baharini"


Card image
Commodore: Hassan Mussa Mzee
Card image
Captain: Khamis Simba Khamis
Card image
CDR/Commander: Khamis Taji Khamis

© 2019 Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar - KMKM. Haki zote zimehifadhiwa