Barua pepe: kikosimaalum64@kmkmzanzibar.go.tz  |  S.L.P: 565

Logo
Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar
Logo

Malengo ya KMKM


Madhumuni/Shabaha

Madhumuni ya Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM)
     Madhumuni hasa ya kuanzishwa kwa vyombo hivi vya ulinzi na usalama kikiwemo Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo (KMKM) ni kulinda uhuru wa Zanzibar (ambao ulipatikana kwa njia ya mapinduzi ya 1964) pamoja na watu wake na kulinda mipaka ya baharini ya Zanzibar dhidi ya vitisho na wapinga mapinduzi matukufu ya 1964, pia na kuleta ustawi wa wananchi wote wa Zanzibar.

Malengo

Malengo ya Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM)
     Ni kuwa na Kikosi bora na cha kisasa chenye uwezo wa kulinda mipaka ya bahari ya Zanzibar. Malengo haya yanathibitishwa na kauli ya aliye kuwa Raisi wa kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee. ABEID AMANI KARUME pale alipokuwa akiwaaga vijana wa kundi la kwanza kwa safari ya kwenda mafunzoni nchini Ujerumani Mashariki aliposema ".....Vijana mkasome usiku na mchana maana nchi haina ulinzi wa kutosha baharini"


© 2019 - 2024 Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar - KMKM. Haki zote zimehifadhiwa