Barua pepe: kikosimaalum64@kmkmzanzibar.go.tz  |  S.L.P: 565

Logo
Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar
Logo

Uzinduzi wa Jengo la Ghorofa Mbili la Kituo cha Mama na Mtoto Hospitali ya KMKM Kibweni Mjini Zanzibar


Hospitali ya KMKM Kibweni Mjini Zanzibar

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni Wilaya ya Magharibi ‘A’ Unguja, Jumatatu ya tarehe 07/01/2019, ikiwa ni shamrashamra za miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar 1964.

Hospitali ya KMKM Kibweni Mjini Zanzibar

Makamu wa Rais wa Jamuhuri la Mungano ya Tanzania Azindua Jengo la Ghorofa Mbili la Kituo cha Mama na Mtoto Hospitali la KMKM Kibweni Mjini Zanzibar Ikiwa ni Miongoni mwa Shamra Shamra za Kuadhimisha Sherehe za Miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Watumishi wa afya ya Mama na Mtoto nchini wametakiwa kutanguliza utu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kazi na kuacha tabia ya kutumia lugha isiyonzuri wakati wanapotoa huduma kwa wananchi.

Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa wito huo Kibweni, Wilaya ya Magharibi ‘A’, alipokuwa akizinduwa Jengo la Kituo cha Mama na Mtoto katika Hospitali ya Kikosi cha KMKM ikiwa ni miongoni mwa maadhimisho ya miaka 55 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Alisema kazi ya utowaji wa huduma ya afya ni kazi ya wito inayohitaji moyo wa huruma, upendo na uvumilivu na kubwa zaidi ni kujitahidi katika kusaidia jamii na kutarajia ujira kutoka kwa Mwenyezi mungu.

Aliwashauri wataalamu wa afya kutumia utaalamu wao kutekeleza wajibu mkubwa wa kuwahudumia wananchi na kusaidia kuokoa maisha ya Mama na Mtoto ili kuepuka vifo vitokanavyo na uzazi.

“Ni wajibu wenu kutumia utaalamu wenu na jukumu mlilopewa na Taifa katika kuleta mabadiliko ya kiutendaji na ufanisi katika Sekta ya afya Nchini,” alisema Makamo wa Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliwaahidi wataalamu wa huduma ya afya ya Mama na Mtoto kupatiwa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kila fursa itakapopatikana ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuwaongezea utaalamu zaidi.

Aidha alisema uamuzi wa kuimarishwa kwa huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni ni jambo la faraja katika Sekta ya afya kwani itasaidia kupunguza msongomano katika hospitali ya Mnazi mmoja na Muembeladu.

Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa huduma ya Mama na Mtoto katika Hospitali ya KMKM Kibweni kitawapunguzia usumbufu wananchi kufuata huduma hiyo hospitali za mbali na itapunguza idadi ya vifo vya Mama na Mtoto ambavyo ni vikubwa kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Shirika la Afya Duniani WHO.

Aliwaomba watendaji na Wananchi watakaofika kwa ajili ya kupatiwa huduma kujenga utamaduni wa kuimarisha usafi wa jengo na kuvitunza vifaa vitakavyotumika ili viweze kudumu kwa muda mrefu.

Mapema akisoma taarifa ya kitaalamu ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jingo hilo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Bi. Radhiya Rashid Haroub alisema kujengwa hospitali ya KMKM Kibweni ni kuimarisha huduma za afya ya Mama na Mtoto na kuwahudumia wananchi wa maeneo ya karibu na hospitali hiyo.

Alisema kuwepo kwa hospitali hiyo kutaipunguzia mzigo hospitali ya Mnazi mmoja hasa kwa maradhi ya kawaida pamoja na kukuza uhusiano mazuri baina ya Kikosi cha KMKM na Wananchi.


© 2019 - 2023 Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar - KMKM. Haki zote zimehifadhiwa