Barua pepe: kikosimaalum64@kmkmzanzibar.go.tz | S.L.P: 565
Timu ya KMKM Zanzibar Yatangazwa Bingwa Kwa Msimu wa Mwaka 2018 /2019 Ligi Kuu ya Zanzibar Iliofika Tamati tarehe 29 April 2019 Katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
Kamishna wa Michezo Zanzibar Bi. Sharifa Khamis akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar Nahodha wa Timu ya KMKM Makame Haji Ngwali, baada ya kukamilisha mchezo wake wa mwisho na Timu ya JKU, na Kutangazwa Bingwa kwa mwaka 2018/2019 katika Uwanja wa Amaan Zanzibar.
MABINGWA wapya wa ligi kuu ya Zanzibar KMKM wamekabidhiwa kombe lao rasmi baada ya kukamilisha mechi yao ya mwisho Kati yao na JKU.
KMKM wamefanikiwa kutwaa ubingwa huo baada ya kufikisha pointi 80 ubingwa ambao walioukosa karibu miaka mitano.
Kombe hilo walikabidhiwa na kamishna wa Michezo Sharifa Khamis ambae alikuwa mgeni rasmi wa mchezo huo wa kumalizika ratiba kwa timu zote.
Katika mchezo huo KMKM walianza kuandika bao la Kwanza mnamo dakika ya 34 kupitia kwa mfungaji wake Mussa Ali Mbarouk ambalo lilidumu Hadi mapumziko.
KMKM ambao walitangulia kupata ubingwa huo wakiwa na mchezo mmoja mkononi waliingia kipindi cha pili na kuendelea kuliandama lango la wapinzani wao hao.
Bao la pili la KMKM lilifungwa tena na Mussa Ali Mbarouk ambae amefikisha bao la 23 na kutangazwa kuwa mfungaji Bora na Abuubakar Khamis Sufiani wa zimamoto ambae nae alifunga idadi Kama hiyo lakini alitangazwa kuwa mchezaji Bora.
Kikosi maalum cha kuzuia magendo (KMKM) cha fanya mashindano ya mbio za kilomita 10 Zanzibar. Mgeni rasmi katika mashindano hayo ya riadha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serekali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh. Haji Omar Kheri.
Washiriki wa mashindano ya KMKM kilomita kumi wanawake na wanaume, wakisubiri kuanzishwa kwa mbio hizo katika mashindano yaliyoanzia Makao Makuu ya kikosi hicho Kibweni na kumalizikia Maisara mjini Zanzibar.
Wakimbiaji katika mashindano ya kilomita kumi yaliyoandaliwa na kikosi cha KMKM wakichuana vikali kuelekea mfundani.
Mkimbiaji Nelson Priver wa timu ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Arusha akifuatiwa na John Leonard pia wa timu hiyo wakiongoza mashindano hayo.
Mkimbiaji Sarah Ramadhan kutoka Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), akimaliza mashindano hayo kwa kushika nafasi ya kwanza kwa upande wa wanawake katika viwanja vya Maisara.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo ya riadha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serekali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh. Haji Omar Kheri (wa 5 kutoka kulia) akijumuika na viongozi wengine kuwashangiria wanariadha waliokuwa wakipita mbele yao.
Mjumbe wa kamati ya maandalizi ya KMKM kilomita kumi CPO. Abdallah Shaaban akisoma risala ya mashindano kwa mgeni rasmi na wageni walikwa waliohudhuri katika mashindano hayo.
Mkimbiaji mkongwa aliyoipa sifa Tanzania Kanali Mstaafu. Juma Ikangaa akitaa nasaha zake kwa wakimbiaji wa mbio za KMKM kilomita kumi mara tu baada ya kumalizika kwa mashindano hayo.
Mkuu wa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM) Comodore Hassan Mussa akitoa shukrani kwa washiriki wote wa mashindano yaliyoandaliwa na kikosi chake na kumkaribisha mgeni rasmin.
Mgeni rasmi katika mashindano hayo ya riadha, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa, Serekali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Mh. Haji Omar Kheri akiwahutubiwa wanamichezo waliomaliza mashindano ya KMKM kilomita kumi katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Mgeni rasmi katika mashindano ya KMKM kilomita kumi Waziri. Haji Omar Kheri akimpa zawadi ya pesa taslim laki tano mshindi wa kwanza kwa upande wa wanawake Sarah Ramadhan.
Mgeni rasmi katika mashindano ya (KMKM) kilomita kumi Waziri. Haji Omar Kheri (katikati) waliosimama chini, (kulia) Waziri wa Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo Rashid Ali Juma na (kushoto) Mkuu wa Kikosi cha KMKM Komodoo. Hassan Mussa wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa 1, 2 na 3 wa mashindano ya KMKM kilomita kumi.
© 2019 - 2023 Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar - KMKM. Haki zote zimehifadhiwa