Barua pepe: kikosimaalum64@kmkmzanzibar.go.tz  |  S.L.P: 565

Logo
Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar
Logo
Historia Fupi ya Kikosi Maalum Cha Kuzuia Magendo Zanzibar (KMKM)

Baada ya Mapinduzi Matukufu ya 1964, ambayo yaliongozwa na Chama Cha Afro Shirazi Party (ASP) chini ya Jamadari wa Mapinduzi na Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee Abeid Aman Karume, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilianzisha vyombo vya ulinzi na usalama ambavyo ni JESHI LA UKOMBOZI (JLU), Idara ya Usalama wa Zanzibar na kuimarisha Jeshi la Polisi.
Kikosi cha Wanamaji Zanzibar (Zanzibar Navy) ambacho asili yake ni Idara ya Usalama Zanzibar kilikuwa na malengo ambayo ni kulinda uhuru wa Zanzibar (ambao ulipatikana kwa mapinduzi ya 1964) pamoja na mipaka ya baharini ya Zanzibar na watu wake.
Mnamo tarehe 01/07/1973 Kikosi cha Wanamaji Zanzibar kubadilishwa jina na kuitwa Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo (KMKM), mbali ya kubadilishwa jina lakini malengo na madhumuni yake yalibaki kuwa yale yale.
Mwaka 1984 Kikosi cha Wanamaji Zanzibar (Zanzibar Navy) kiliondolewa kutoka Idara ya Usalama Zanzibar na kuwa kikosi kinachojitegemea. Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 1984 inaeleza kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ndiye Kamanda Mkuu wa kikosi hicho na vyengine vilivyoundwa na vitakavyoundwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kisiwa cha Unguja
Paris

Ramani ya Kisiwa cha Unguja

Zanzibar ni mkusanyiko wa visiwa vikubwa viwili vya unguja na Pemba, pia vikipakana pembezoni mwake na visiwa vyengine vidogo vidogo kama Changuu. Misali, Pungume na kadhalika.
Zanzibar ni visiwa vinavyopatikana katika bahari ya Hindi, ni visiwa ambavyo vimebarikiwa neema nytingi hususan matunda na nafaka toifauti, pia ina mandahari nzuri kutokana nafukwe zake pamoja na mji wa kihistoria wa mji mkongwe.

Kisiwa cha Pemba
Paris

Ramani ya Kisiwa cha Pemba

Zanzibar ni mkusanyiko wa visiwa vikubwa viwili vya unguja na Pemba, pia vikipakana pembezoni mwake na visiwa vyengine vidogo vidogo kama Changuu. Misali, Pungume na kadhalika.
Zanzibar ni visiwa vinavyopatikana katika bahari ya Hindi, ni visiwa ambavyo vimebarikiwa neema nytingi hususan matunda na nafaka toifauti, pia ina mandahari nzuri kutokana nafukwe zake pamoja na mji wa kihistoria wa mji mkongwe.

Picha za Maafisa waliowahi kuwa wakuu wa KMKM

historia1
Commodore: Azanna Hassan Msingiri
historia1
Commodore: Hassan Mussa Mzee
historia2
......................................

© 2019 - 2023 Kikosi Maalum cha Kuzuia Magendo Zanzibar - KMKM. Haki zote zimehifadhiwa